Dar es Salaam, Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania leo imetangaza kubadilisha huduma yake ya fedha ya M-Pesa kutoka teknolojia ya awali ya G1 kwenda mpya ya G2, lengo kubwa ikiwa ni kuboresha huduma hii kwa kuiingiza katika teknolojia ya juu ili iweze kupatikana wakati wowote kwa uhakika na kwa kasi kubwa wakati wa ufanyaji wa mihamala ya malipo na huduma mbalimbali.

Matumizi ya teknolojia mpya ya G2 ambayo miundombinu yake imejengwa hapa nchini itarahisisha matengenezo yake pindi yatakapojitokeza matatizo ya kimtandao pia itawezesha kupanuka kwa matumizi ya huduma hii kwenye kuboresha na kuunganisha  huduma mbalimbali na kibiashara.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa matumizi ya teknolojia hii mpya katika hafla iliofanyika leo,Afisa Mtendaji Mkuu wa huduma za malipo ya mtandao wa Vodacom Tanzania, Sitoyo Lopokoiyit amesema “Tunawaletea huduma ya M-pesa katika teknolojia mpya na bora zaidi,tunajivunia kwa kazi  nzuri iliyofanyika kufanikisha mabadiliko haya ambayo yatawawezesha watanzania kupata huduma bora za kifedha kupitia huduma ya M-Pesa iliyoboreshwa zaidi.Ubunifu na matumizi ya teknolojia hii mpya yataboresha huduma hii sio kwa wateja wa Vodacom pekee bali biashara mbalimbali na huduma zinazofanyika kupitia huduma hii”
Sitoyo aliongeza kusema kuwa teknolojia hii  italeta mapinduzi makubwa ya matumizi ya huduma za kifedha kwa njia ya mtandao wa simu na Vodacom itaendelea kujenga mazingira ya kukuza biashara za malipo kwa njia ya mitandao na kuzidi kuiweka Tanzania mbele katika huduma za biashara kwa njia ya mtandao pia kuongeza wigo wa huduma za kimtandao kama vile kuweka akiba,kuchukua na kulipa mikopo,ufanyaji wa mihamala ya malipo kwa mtandao,huduma za bima na huduma nyinginezo nyingi tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Huawei,Bruce Yang alisema “Kupitia teknolojia ya kiwango cha juu ya Huawei,Huduma za M-Pesa zimebadilika kabisa na kuwa za kiwango kikubwa cha ubora na imeboreshwa zaidi kuweza kukidhi matakwa ya huduma mbalimbali za kifedha.Kwa kutumia timu ya wataalamu wetu tumeweza kujenga miundombinu ya kisasa itakayowawezesha watanzania kupata huduma za kifedha kwa viwango vya kimataifa.Tumefurahishwa na ushirikiano tulioupata kutoka timu nzima ya wafanyakazi wa Vodacom hali iliyotuwezesha kumaliza mradi huu wa kubadilisha teknolojia mapema tofauti na jinsi tulivyotegemea” 
Huduma ya M-Pesa ya Vodacom Tanzania ikiwa ni ya kwanza kwa kutuma , kupokea fedha na kufanya mihamala mbalimbali ya malipo inaaminika kwa watanzania wengi.Tangia ianzishwe katika kipindi cha miaka 8 iliyopita inao watumiaji wapatao milioni 9.Kupitia teknolojia hii mpya ya G2,huduma za M-Pesa zimeboreshwa kuwa nzuri na  ubunifu wa kutumiwa kwa malipo,  huduma mbalimbali na kuwa na uwezo wa kuunganisha biashara .Mabadiliko haya ni ya kihistoria katika huduma za kifedha kwa njia ya simu nchini Tanzania na kampuni inawahaidi watumiaji wategemee ubunifu wa kila aina kwa matumizi ya huduma hii katika teknolojia hii  ambayo kuanza kwake kutumika nchini  ni mafanikio makubwa katika kuboresha huduma  za kifedha kwa watanzania . Vodacom Tanzania inajivunia kufanikisha kuleta teknolojia hii ambayo inategemewa kuleta  mapinduzi makubwa ya huduma za kifedha nchini.
For English version CLICK HERE

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...