THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.UJUMBE KUTOKA IKULU

video


Mwenge Jazz Band wana paselepa bado wapo gado sana tu


MICHUZI TV: HOSPITALI YA HAYDOM KUPANDISHWA HADHI - WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA


MICHUZI TV: TAKWIMU YA MAJANGA YA MOTO MKOA WA MBEYA KWA MIAKA SITA ILIYOPITA


MICHUZI TV: MAHAKAMA KUU YAMWEKEA ZUIO LA MUDA MHE. FREEMAN MBOWE


DKT. KIGWANGALLA ATEMBELEA VITUO VYA TIBA YA DAWA ZA KULEVYA

Naibu wa Waziri wa Afya Dkt. Kigwangalla afanya ziara ya kushtukiza kwenye kituo cha kuwahudumia watu wanaotibiwa kuacha dawa za kulevya kwa kutumia methadone kilichopo Hospitali ya Mwananyamala ili kuona namna huduma zinavyotikewa. 

Ameamua kufanya ziara hiyo sababu kuna ongezeko kubwa la wateja siku za hivi karibuni kutokana na kuongezeka udhibiti. Na kuna taarifa kwamba wanaouza dawa za kulevya (drug dealers) wameathiriwa sana kwa kupoteza mapato ya sh bilioni 70 kwa uwepo wa vituo hivi ambavyo kwa sasa vinahudumia wateja 3351, na hivyo wameanza kubuni mbinu za kuwarudisha kwenye matumizi ya dawa za kulevya kwa mbinu mbalimbali ikiwemo kudai kuwa methadone haifanyi kazi.

Dkt. Kigwangalla ameagiza:

1. Hospitali zote za kanda zianzishe vituo vya rehab ndani ya miezi 6

2. Hospitali zote za mikoa nchini zianzishe kliniki ya kutoa methadone ndani ya miezi 6

3. Katibu Mkuu afya ahakikishe kuna Daktari bingwa wa afya ya akili kwenye kila mkoa ili kuanzisha na kusimamia vituo vya kutoa tiba ya methadone

4. Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kinondoni aongeze eneo la kliniki sambamba na watumishi kwenye kituo hiki 

5. Kamishna wa polisi wa operesheni maalum afuatilie wateja (exit follow-up) wanaotoka kliniki ili kudhibiti mkakati wa drug dealers wanaolenga kuwarubuni na kuwarudisha kwenye dawa za kulevya wateja wa vituo hivi. 

Msafara wa Dkt. Kigwangalla umeelekea Temeke Hospitali kwenye kituo kingine kama hiki.


MSAADA UNAHITAJIKA KWA MTOTO CATHERINE

Mzazi wa mtoto Catherine anaomba msaada wako wa hali na mali kumuweza mtoto huyu mwenye ulemavu aweze kulipa ada yake ili aendelee na masomo . Mtoto huyu anasoma shule ya St. Bernard, lakini kutokana na mama yake kutokuwa na uwezo hivi sasa wa kulipa ada mtoto yuko nyumbani. Mama wa mtoto huyu Flora anaomba wasamaria wema kuweza kumsaidia kulipa ada ya mtoto ili aweze kurudi shuleni. Kwa wale walioguswa mnaweza kutuma msaada kwa kupitia akaunti ya Evelyn Kamukuru 0112014797900 CRDB BANK


KANALI MSTAAFU NGEMELA LUBINGA AMTEMBELEA NAIBU WAZIRI MASAUNI OFISINI KWAKE JIJINI DAR ES SALAAM

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga, alipomtembelea kujadili masuala mbalimbali yaliyohusiana na utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi Mkuu uliopita. Mazungumzo hayo yamefanyika ofisini kwa Naibu Waziri, jijini Dar es Salaam.Katikati ni msaidizi wa Katibu huyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga,akizungumza na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati wa mazungumzo mbalimbali yaliyohusiana na utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi Mkuu uliopita.Mazungumzi hayo yamefanyika ofisini kwa Naibu Waziri,jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akifafanua jambo kwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Siasa na mahusiano ya Kimataifa,Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga, alipomtembelea kujadili masuala mbalimbali yaliyohusiana na utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi Mkuu uliopita.Mazungumzi hayo yamefanyika ofisini kwa Naibu Waziri,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi


KITUO CHA FORODHA CHA MPAKA WA TUNDUMA/NAKONDE (TANZANIA NA ZAMBIA) CHAANZA KUFANYAKAZI


Benny Mwaipaja, WFM, Tunduma

KITUO cha Pamoja cha Forodha cha mpaka kati ya Tanzania na Zambia (Tunduma/Nakonde) kimeanza rasmi kutumika licha ya kukabiliwa na msongamano mkubwa wa magari unaotakiwa kupatiwa ufumbuzi wa haraka.

Kituo hicho kimeanza kufanyakazi tangu Februari mosi mwaka huu, ambapo watumiaji wa mpaka huo watakuwa wakihudumiwa upande mmoja wa mpaka badala ya utaratibu uliokuwa ukitumika awali ambapo watumiaji walilazimika kukaguliwa mizigo yao kila upande hatua iliyokuwa ikichelewesha biashara katika mpaka huo

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda na Naibu Waziri wa mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahya, wameeleza kuridhishwa na kazi inayofanyika mpakani hapo kupitia mfumo huo mpya.

Hata hivyo baadhi ya madereva wanaosafirisha bidhaa kupitia mpaka huo wa Tunduma na Nakonde, pamoja na kupongeza utaratibu huo mpya, wameiomba Serikali iwasiliane na upande wa Zambia, ili waongeze kasi ya kuruhusu malori kuendelea na safari yanapofika mpakani hapo bila kucheleweshwa ili kwenda sambamba na kasi ya upande wa Tanzania, ambao umeboresha kwa kiwango kikubwa utoaji wa huduma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda, amesema kuwa makubaliano yaliyofikiwa kati ya Serikali na watoa huduma katika mpaka huo yalikuwa ni kuwahudumia wadau wanaotumia mpaka huo kwa muda usiozidi siku moja na kuwataka madereva wa malori wanaokwazwa kuwasiliana na mamlaka zinazohusika.
Kaimu Afisa Uhamiaji Mfawidhi wa Kituo cha mpakani Tunduma/Nakonde, Bw. Tabaran Mzee, (aliyevaa sare za uhamiaji), akieleza namna idara hiyo ilivyoanza utekelezaji wa uanzishwaji wa Kituo cha Pamoja cha Forodha kati ya Tanzania na Zambia, ambapo wafanyakazi wa idara hizo kutoka nchi hizo mbili wanafanyakazi katika jengo moja kila upande wa nchi ili kuboresha ufanyaji biashara mpakani.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji (anayeshughulikia biashara na uwekezaji), Prof. Adolf Mkenda, akionesha kibao chenye namba za simu kilichowekwa Idara ya Forodha katika mpaka wa Tunduma/Nakonde zitakazotumiwa na wadau endapo watakuwa na malalamiko yoyote, lengo likiwa ni kuboresha huduma katika mpaka huo ambapo huduma ya pamoja ya forodha kati ya Tanzania na Zambia imeanza kutolewa rasmi tangu Februari mosi mwaka huu.
Makatibu Wakuu wa Wizara ya Fedha, Viwanda, na Mambo ya Ndani, wakizungumza na Afisa Forodha wa Zambia aliyeko katika Kituo cha Forodha cha Tunduma upande wa Tanzania, baada ya Ujumbe huo wa Serikali kutembelea mpaka huo kukagua shughuli za biashara ikiwa ni siku kadhaa baada ya kuanza rasmi kwa huduma ya Kituo cha Pamoja cha Forodha katika mpaka huo wa Tunduma/Nakonde (Tanzania na Zambia).
Mkuu wa Wilaya ya Momba mkoani Mbeya Bw. Juma Irando (aliyenyoosha kidole) akieleza jambo baada ya ujumbe wa Serikali ukiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban, ulipotembelea mpaka huo kukagua shughuli za biashara baada ya kuanza rasmi kwa huduma za Kituo cha Pamoja cha Forodha mpakani Tunduma/Nakonde.
Kituo cha Uhamiaji na Forodha cha Tanzania kilichoko kwenye jengo la Zambia upande wa Nakonde, baada ya kuanzishwa kwa Kituo cha pamoja cha Forodha cha Mpakani mwa Tanzania na Zambia (Tunduma/Nakonde).


KATIBU WA NEC IDARA YA SIASA NA UHUSIANO WA KIMATAIFA CCM KANAL MSTAAFU NGEMELA LUBINGA ATEMBELEA UVCCM OFISI NDOGO DAR ES SALAAM LEO.Kaimu katibu UVCCM Shaka Hamdu Shaka wa pili kulia akimuonyesha ofisi mbalimbali Katibu wa NEC Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga mara baada ya kuwasili Ofisi Ndogo Makao Makuu ya UVCCM Taifa

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka akitoa ufafanuzi na kumkaribisha Katibu wa NEC Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga kuzungumza na wajumbe Wa Sekretariet Ya UVCCM TAIFA pamoja na wafanyakazi Ofisi Ndogo Makao makuu Uvccm Dar es Salaam.

Katibu wa NEC Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu
Ngemela Lubinga akizungumza Wajumbe Sekretariet Ya UVCCM TAIFA pamoja na wafanyakazi Ofisi Ndogo Makao makuu Uvccm Dar es Salaam.

picha ya Pamoja ya Katibu wa NEC Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga pamoja na Wajumbe wa Sekretariet Ya UVCCM TAIFA Ofisi Ndogo Makao makuu Uvccm Dar es Salaam.SBL yaanza kuuza bia Kenya

Kwa mara ya kwanza, Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imeanza kuuza nje ya nchi bidhaa zake katika soko la kikanda, eneo la kwanza likiwa ni nchi jirani ya Tanzania kwa upande wa Kaskazini, Kenya.

Shehena ya kwanza ya bia inayofahamika kama Allsopps ilisafirishwa kwenda Kenya wiki iliyopita na hivyo kukiweka kiwanda cha SBL kuwa mmoja wachangiaji wakubwa katika soko la kanda.

Akizungumzia kuhusu hatua hiyo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL, John Wanyancha alisema; “Hii ni hatua nyingine ya kufurahisha katika kampuni yetu na kimsingi kwa bidhaa zetu. Ukweli unabakia kwamba kumudu kupenyeza ndani ya soko la Kenya kunaonesha kuwa ubora wa bidhaa zetu sio tu kwamba unakubalika na wateja wetu wa ndani bali pia zinakubalika katika soko kubwa la kikanda.”

Wanyancha alisema kuwa SBL inaangalia uwezekano wa kupanua mauzo ya biashara katika masoko mengine ya kikanda, hatua ambayo iko katika mkondo wa kuhamasisha Jumuia ya Afrika Mashariki na kada nyingine za kiuchumi kuongeza biashara yake ya kuvuka mpaka ndani ya ukanda huo.

SBL imekuwa inazalisha aina za bidhaa zinazotambulika kimataifa kama vile Pilsner Lager,Tusker Lager, TuskerLite, Kibo Gold, Guinness Stout, Uhuru, The Kick pamoja na bidhaa kuu ya Serengeti Premium Lager-ambayo peke yake imeshajizolea medali kumi zinazotambuliwa kimataifa. 


WASTAAFU WANAOLIPWA NA HAZINA WAJITOKEZA KUHAKIKIWA ZANZIBAR-WAILIIA SERIKALI IWAONGEZE PENSHENI


Benny Mwaipaja, WFM, Zanzibar

MAMIA ya wastaafu wa Taasisi za Muungano kutoka visiwa vya Pemba na Unguja-Zanzibar, wanaolipwa na Wizara ya Fedha na Mipango ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wamejitokeza kwa wingi kuhakikiwa huku wakiiomba Serikali iwaongezee pensheni kutokana na wengi wao kukabiliwa na hali ngumu ya maisha.

Wakizunguza katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango-Zanzibar, iliyoko katika eneo la Vuga, wastaafu hao wamepongeza hatua ya Serikali ya kuwahakiki ili kufahamu hali zao na kwamba hatua hiyo itasaidia kuwabaini watu wasio na sifa ya kupata malipo hayo kutoka Serikalini

Wastaafu Bi Sauda Ramadhani Mpambalyoto na Abuu Ali Hamisi, wameiomba Serikali iangalie namna ya kuwaongezea pensheni wataafu ambao wengi wao ni wagonjwa hawajiwezi na wengine wana afya njema, wanalima, lakini wanahitaji kuwezeshwa na Serikali ili waweze kumudu maisha ambayo wamesema yamepanda.

Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Msaidizi, Bw. Stanslaus Mpembe, amesema kuwa Wizara ya Fedha na Mipango inaendesha zoezi la kuhakiki wastaafu wanaolipwa pensheni na wizara hiyo ili kuhuisha taarifa za wastaafu kwa lengo la kupata kanzidata (database) iliyo ili kuiwezesha Serikali kuwalipa wastaafu wanaostahili.
Mkaguzi wa Ndani kutoka Wizara ya Fedha na Mipango-Bara, Bw. Paison Mwamnyasi (aliyenyoosha mkono) akitoa maelekezo kwa wastaafu wanaolipwa pensheni zao na Wizara ya Fedha na Mipango ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, waliofika katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango-Zanzibar, eneo la Vuga, kwa ajili ya uhakiki.
Zoezi la uhakiki likiwa linaendelea katika ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar, kulia ni mstaafu Bw. Amir Apacho akifanyiwa uhakiki na Mkaguzi Bi. Mary Mauki.
Mchambuzi mwandamizi wa mifumo ya kompyuta Bi. Magreth Ambrosi Akipokea namba kutoka kwa mstaafu (aliyeko dirishani) aliyopewa kwa ajili ya uhakiki. Uhakiki wa Wastaafu unafanyika katika ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango-Zanzibar, katika eneo la Vuga.
Baadhi ya wastaafu ambao ni wagonjwa wakisubiri kupata huduma wakiwa wametengewa sehemu maalumu kwa ajili ya kupata huduma hiyo ya uhakiki.
Afisa Tehama wa Wizara ya Fedha na Mipango akimfanyia uhakiki Bw Uleja Edward katika ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango-Zanzibar, zilizoko eneo la Vuga visiwani humo.
Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko-Zanzibar, Mhe. Balozi Amina Salum Ali, alipowasili katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango-Zanzibar kwa ajili ya kufanyiwa uhakiki. Aliyesimama mbele yake ni Mkaguzi wa Ndani Bw. Nicholaus Jalane.CALL FOR PAPERS: 9th Mwalimu Julius Nyerere Intellectual Festival, University of Dar es Salaam, TanzaniaKATIBU MKUU WA MAMBO YA NJE AFUNGUA KIKAO CHA MAKATIBU WAKUU WA SADC-ISPDC

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Aziz P. Mlima, akifungua Mkutano cha Makatibu Wakuu nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa Kamati Ndogo ya Mawaziri ya Siasa na Diplomasia ya SADC (Inter State Politics and Diplomacy Sub Committee-ISPDC) unaotarajiwa kufanyika tarehe 23 na 24 Februari, 2017. Mkutano wa Makatibu Wakuu unafanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. 
Sehemu ya wajumbe wa Mkutano kutoka katika mataifa ya nchi wanachama wakifuatilia mkutano. 
Kaimu Mkuu wa Mabalozi Mhe. Balozi Edzai Chimonyo (wa kwanza kushoto) na wajumbe wengine wakifuatilia mkutano.
Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Dkt. Stergomena Tax (wa pili kushoto) na wa kwanza kulia ni Balozi Simba Yahya, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakifuatilia mkutano. 
Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia Mkutano. 


MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM PAUL MAKONDA AKABIDHIWA HEKALI 1500 NA AZIMIO HOUSING ESTATE LEO

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amekabidhiwa hekali 1500 na Mkurugenzi wa Azimio Housing Estate Mohamed Iqbal kwa ajili ya viwanda vidogo.

Akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo  eneo la Kisarawe II wilaya ya Kigamboni Mkurugenzi huyo amesema wameamua kumkabidhi eneo hilo RC Makonda kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli za kuijenga Tanzania ya viwanda ili kuwakomboa wananchi wenye uchumi wa kati.

Kwa upande wake RC Makonda ameeleza kuwa dhamira ya viwanda ya Rais Magufuli inabidi itafsiriwe kwa vitendo, hivyo eneo hilo litatumika kwa ajili ya ufugaji, kilimo, usindikaji, utengenezaji wa sabuni na eneo hilo litatumika na wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam.

Pia RC  Makonda ameongeza kuwa Mkoa wa Dar es Salaam unajengwa na wana Dar es Salaam wenyewe hivyo kama kuna watu wanataka kujitolea kwa ajili ya maendeleo ya Dar es Salaam wafanye hivyo.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul  Makonda akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya makabidhiano hayo  eneo la Kisarawe II wilaya ya Kigamboni leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul  Makonda akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul  Makonda akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa wakiangalia ramani ya eneo hilo, leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe: Paul Makonda  (watatu kutoka kulia)  akiwa amefuatana na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa, na Mkurugenzi wa Azimio Housing Estate,Mohamed Iqbal    wakikagua eneo hilo
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda  akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa,
Muomoneke wa  eneo hilo alilokabidhiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii. 


TAKWIMU YA MAJANGA YA MOTO MKOA WA MBEYA KWA MIAKA SITA ILIYOPITA


SGT Weston Paul Ngaponda akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari wakati akijibu maswali yaliyoulizwa na Bw. Fadhiri Aticki Mr Pengo kutoka Michuzi Blog na Michuzi Tv.

Jeshi la Zimamoto Mkoa wa Mbeya limetoa Takwimu ya Ajali za Moto zilizotokea ndani ya miaka 6 kuanzia 2011 mpaka 2016.
Akizungumza na waandishi wa habari Sajenti Weston Paul Ngaponda kwa niaba ya Mkuu wa Operesheni Zimamoto Mkoa wa Mbeya amesema Jeshi la Zimamoto na Uokozi Mkoani Mbeya linafanya majukumu yake kwa weredi mkubwa na kwa mafanikio makubwa.


SGT Ngaponda ametoa Takwimu za Ajali za moto kwa muda wa miaka sita na zipo kama ifuatavyo:-
1.Mwaka 2011,Matukio ya Moto yalikuwa  jumla 54 kwa wastani wa Matukio matano kwa mwezi.
2. Mwaka 2012, kwa mwaka mzima matukio yalikuwa jumla 88, kwa wastani wa matukio 7 kila mwezi.
3. Mwaka 2013, Jumla ya matukio ya moto yalikuwa 50, kwa wastani wa matukio manne kila mwezi.
4. Mwaka 2014, Jumla ya matukio ya moto yalikuwa 52, kwa wastani wa matukio manne kila mwezi.
5. Mwaka 2015, Jumla ya matukio ya moto yalikuwa 74, kwa wastani wa matukio 6 kila mwezi.
6. Mwaka 2016, Jumla ya matukio ya moto yalikuwa 65, wastani wa matukio matano kila mwezi.
SGT Ngaponda akiongea na wanaHabari amesema kwa tathmini zao ni kwamba matukio ya ajali za moto yanazidi kupungua Mkoani Mbeya huku akiwasifu wananchi kwa ushirikiano wanaowaonyesha pindi majanga ya moto yatokeapo. Aidha,SGT Ngaponda amesema Jeshi la Zimamoto limekuwa likitoa elimu kuhusu majanga ya moto pindi litokeapo tatizo sehemu ili kusaidia kupunguza hatari hizi kwa siku za usoni. Pia amesema vyanzo vya moto daima husababishwa na binadamu kwa mitazamo tofauti, inaweza kuwa kwa Ujinga, Uzembe na Uhujumu.
Akitolea maelezo jinsi ya kuepuka majanga ya moto amesema, kwa wale wazembe basi Umakini unahitajika sana pindi watumiapo vitu vinavyoweza kusababisha moto kama mishumaa, taa ya kandiri, matumizi ya umeme na kwa upande wa Ujinga Elimu pekee inaweza kusaidia kuifanya jamii kuwa salama zaidi. SGT Ngaponda amewaomba wananchi wa Mkoa wa Mbeya kujitahidi kutoa taarifa mapema majanga yatokeapo bila kuchelewa kwani wapo wananchi ambao huchelewa kutoa taarifa.
Akihitimisha Taarifa hiyo ametoa wito kwa wananchi hasa waiishio Mbozi kwani wamekuwa na tabia ya udanganyifu kwa kuwapigia simu Jeshi la Zimamoto kuwa kuna janga la Moto kumbe sio kweli na baadhi ya wananchi kuzitumia namba za Zimamoto kwa matumizi yasiyostahiki.
 Wanahabari wakimsikiliza kwa makini SGT Ngaponda wakati akitoa Ufafanuzi juu ya masuala mbalimbali yahusuyo Jeshi la Zimamoto
MAELEZO NA: THOBIAS OMEGA
PICHA NA: MR PENGO MMG...


WAZIRI MKUU AENDELEA NA ZIARA MKOANI MANYARA LEO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi ya Katesh wilayani Hanang, Mkoani Manyara leo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifanya uzinduzi wa madarasa ya shule ya Msingi ya Mogitu Wilayani Hanang Mkoani Manyara leo, wakati akiendelea na ziara yake ya kikazi mkoa wa Manyara. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananchi wa Hanang Mkoani Manyara baada ya kuzindua madarasa ya shule ya Msingi ya Mogitu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya wananchi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia ngoma ya asili.


WIMBO WA TAIFA WAZUA MJADALA BARAZA LA MADIWANI JIJI LA DAR ES SALAAM

 Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani wa jiji.

Tatizo la wimbo wa Taifa na dua katika mkutano wa baraza la madiwani wa mkoa wa jiji la Dar es Salaam umeweza kuzua mjadala kwa zaidi ya dakika kumi katikati ya mkutano huo.

Mjadala huo ambao uliibuliwa na mtoa hoja, Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea ambaye alitoa hoja ya kukiukwa kwa kanuni za uendeshwaji wa baraza hilo.
  
Mara baada ya kutoa hoja mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam,Sipora Liana alimuomba mwanasheria wa halmashauri kutoa ufafanuzi juu ya swala hili na kusema kuwa hakuna kitu kilichoharibika jambo ambalo lilipingwa vikali na madiwani wote.

Mara baada ya madiwani kumpinga mwanasheria huyo na Mstahiki meya waliamuliwa na madiwani hao kurudia kuimba wimbo wa taifa kisha kufuatiwa na dua jambo ambalo liliridhia kuanza kwa mkutano huo bila mgogoro.

Hoja nyingine aliyoibua kubenea ilikuwa ni kitendo cha kuanzishwa kwa mkutano huo bila ya akidi kutimia na kumlazimu kurudia tena kuhesabu watu ili kujiridhisha kuwa akidi imetimia.

Hata hivyo dakika chache baadae mkutano ulivyoanza ulikuwa kwa majibizano ya hoja mbalimbali ikiwemo juu ya namna uwasilishaji wa taarifa hiyo.

Hata hivyo baraza hilo lilimalizika kwa Meya wa jiji Isaya Mwita kuairisha mkutano mpaka kesho.
 Mbunge wa Ubungo na Diwani wa Baraza la Madiwani wa Jiji la Dar es Salaam , Saed kubenea akizungumza wakati wa kikao cha baraza
 Diwani wa kata ya Kibonde Maji , Abdalah Mtinika akitoa hoja katika kikao cha baraza la Madiwani kilichafanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam
Mayor wa Halmashauri wa Manispaa ya Temeke, Abdalah Chaurembo akitoa hoja katika kikao cha baraza la Madiwani wa jiji la Dar es Salaam
Madiwani wakiwa katika kikao baraza la Madiwani wa jiji la Dar es Salaam katika ukumbi wa Karimjee.


WADAU WA SEKTA YA FILAMU WAKUTANA NA VIONGOZI WA WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO KUJADILI SERA YA FILAMU

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kushoto) akizungumza na wadau wa sekta ya filamu (hawapo pichani) wakati wa kikao cha wadau kuzungumzia sera ya filamu leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura na Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi. Nuru Millao.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akifafanua jambo wakati wa kikao cha wadau wa sekta ya filamu kuzungumzia sera ya filamu leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza akitolea ufafanuzi maoni yaliyotolewa wakati wa kikao cha wadau wa sekta ya filamu kuzungumzia sera ya filamu leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa sekta ya filamu wakisikiliza hoja zilizokua zikiendelea kutolewa wakati wa kikao cha wadau kuzungumzia sera ya filamu leo Jijini Dar es Salaam.