Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa tano kulia), Naibu Balozi wa China Gou Haodong (wa sita kulia) pamoja na wanafunzi waliopata ufadhili kwa ajili ya kusomea fani ya mafuta na gesi asilia katika chuo cha GeoScience (Wuhan).
 Naibu Balozi wa China Gou Haodong (anayezungumza), Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (mbele), wakiwa pomoja na wanafunzi waliopata ufadhili pamoja na waandishi wa habari katika kikao hicho kilichofanyika katika ofisi ya Wizara makao makuu jijini Dar es salaam cha kuwaaga wanafunzi hao.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) na mwanafunzi aliyewakilisha wezake, Mkini Raphael Iddphonce akiwapongeza wanafunzi waliopata fursa hiyo ya kusomea mafuta na gesi asilia nchini china.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) na mwanafunzi aliyewakilisha wezake kwa upande wa wanawake, Salmin Yusra akiongea kwa niaba ya wezake na kuishukuru serikali kwa fursa ya kusomea mafuta na gesi asilia nchini china.


Na Rhoda James
WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo aliwakabidhi Nyaraka za masomo na kuwaaga wanafunzi 18 kati ya wanafunzi 20 mwishoni mwa wiki wanaotarajia kwenda kusomea Shahada ya Uzamivu na ya Uzamili ya Mafuta na Gesi Asilia nchini China.

Profesa Muhongo alisema kuwa, Udhamini huo umetolewa na Serikali ya China na Tanzania, na kuongeza kuwa udhamini huo umekuwa ukitolewa kwa miaka mingi kwa upande wa fani ya Mafuta na Gesi Asilia.

“Udhamini ulianza mwaka 2013-2014 ambapo wanafunzi 10 walipata udhamini huo, mwaka 2014-2015 wanafunzi 10 walipata udhamini, mwaka 2015-2016 wanafunzi 22 walipata na mwaka huu 2016-2017 wanafunzi 20 wamepata udhamini kati ya hao wanafunzi 2 tayari wapo China, ambapo kwa ujumla wanafunzi 62 wameshapata udhamini huo,” alisema Profesa Muhongo.

Profesa Muhongo alisema kuwa wanafunzi hao wameteuliwa kwenda kusoma katika chuo cha China Univesity of Geoscience (Wuhan) na wanatoka mikoa mbalimbali nchini.

“Wanafunzi tunaowachukua sio wa upande wa Mafuta na Gesi asilia tu bali ni wa nyanja mbali mbali ikiwa ni pamoja na Sheria na Fedha,” amesema Profesa Muhongo.

Aidha, alieleza kuwa, Serikali imekuwa ikitoa kipaumbele kwa wanafunzi wa kike kusoma masuala ya mafuta na gesi asilia na mwaka huu, wanafunzi 10 wa kwanza, wa kike waliopata ufadhili kusomea mafuta na Gesi asilia watasomea Shahada ya Uzamili katika chuo cha ‘Geoscience (Wuhan).’

“Nendeni msome kwa bidii bila kujishughulisha na biashara yoyote, kwa kuwa nchi ya Tanzania bado inahitaji wataalamu wa fani ya Mafuta na Gesi asilia,” alisisitiza Profesa Muhongo.

Kwa upande wake Naibu Balozi wa China, Gou Haodong alimshukuru Profesa Muhongo kwa kujali na kuifanya kazi yake kwa ufanisi na kusaidia upatikanaji wa nafasi kwa ajili ya wanafunzi wa Tanzania kwenda kusomea masuala ya Mafuta na Gesi Asilia nje ya nchi.

“Profesa Muhongo amekuwa katika mstari wa mbele katika kutafuta vyuo na ufadhili kwa ajili ya wanafunzi wa Tanzania, hii inaonesha anaipenda kazi yake na anaifanya kwa ufanisi mkubwa,” alisema Naibu Balozi wa China Gou Haodong

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...