Na George Binagi-GB Pazzo

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, amewataka watumiaji wa barabara mkoani Mwanza, kuzingatia sheria za usalama barabarani jambo ambalo litasaidia juhudi za kupambana na ajali kufanikiwa.

Mongella ametoa kauli hiyo hii leo kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani mkoani Mwanza, uliofanyika katika Uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza, ambapo elimu ya usalama barabarani itaendelea kutolewa kwenye maadhimisho hayo kwa juma zima.

Amesema watumiaji wote wa barabara wanao wajibu wa kufuata sheria za usalama barabarani huku akikemea tabia ya baadhi ya abiria wanaowahimiza madereva kuendesha vyombo vyao kwa mwendo kasi.

Kamanda wa Kikosi cha usalama barabarani mkoani Mwanza, Robert Hussein, amebainisha kwamba kwa kipindi cha mwaka jana kati ya mwezi januari na septemba kulikuwa na ajali 161 zilizosababisha vifo 132 na majeruhi 187 na kwamba kwa kipindi kama hicho mwaka huu kulikuwa na ajali 159 zilizosababisha vifo 150 na majeruhi 162 ambapo takwimu hizo zinaonesha kuwepo kwa ongezeko la vifo 18 sawa na asilimia 12 na upungufu wa majeruhi 25 sawa na asilimia 13.3

Baada ya Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani kufanyika Kitaifa mkoani Geita kuanzia Septemba 29 hadi Oktoba Mosi Mwaka huu, Maadhimisho kama hayo kwa mkoa wa Mwanza yamezinduliwa hii leo kwenye Uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza ambapo imeelezwa kwamba bado juhudi za kila mtumiaji wa barabara zinahitajika ili kutokomeza ajali za barabarani.

Kamanda wa Kikosi cha usalama barabarani mkoani Mwanza, Robert Hussein, amebainisha kwamba kwa kipindi cha mwaka jana kati ya mwezi januari na septemba kulikuwa na ajali 161 zilizosababisha vifo 132 na majeruhi 187 na kwamba kwa kipindi kama hicho mwaka huu kulikuwa na ajali 159 zilizosababisha vifo 150 na majeruhi 162 ambapo takwimu hizo zinaonesha kuwepo kwa ongezeko la vifo 18 sawa na asilimia 12 na upungufu wa majeruhi 25 sawa na asilimia 13.3

Pichani juu ni maandamano ya bodaboda pamoja na wa watumiaji wengine wa barabara yakiingia Uwanjani kwenye maadhimisho hayo ambayo yamezinduliwa na Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, akizungumza kwenye uzinduzi wa wiki ya usalama barabarani mkoani Mwanza
Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi, akizungumza kwenye uzinduzi wa wiki ya usalama barabarani mkoani Mwanza
Wanafunzi wa shule ya Msingi Butimba Jijini Mwanza wakiingia uwanjani kuimba wimbo wa kuhamasisha matumizi sahihi na salama ya barabarani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...