Na Editha Karlo,wa blog ya jamii,Kagera.

MARADHI ya vichwa vikubwa na migongo wazi kwa watoto yanatibika endapo wazazi watachukua tahadhali mapema ya kumpeleka mtoto hospitali kwaajili ya matibabu.

Dk Hamis Shaabani daktari bingwa wa upasuaji wa mishipa ya fahamu kutoka Taasisi ya mifupa(MOI) ameyasema hayo leo wakati wa zoezi la ufungaji upasuaji wa vichwa vikubwa na migongo wazi katika hospital ya Mkoa wa Kagera.Dk Hamis alisema kuwa utafiti uliofanywa na Taasisi ya MOI mwaka 2002 unaonyesha zaidi ya watoto 4800 huzaliwa kila mwaka wakiwa na maradhi ya vichwa vikubwa na migongo wazi na kati yao 500 pekee ndiyo wanaoweza kufika hospital na kupatiwa matibabu.

Akizungumzia chimbuko la maradhi hayo Dk Hamisi alisema kuwa watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi wanaweza kuzaliwa nacho au kupata siku chache baada ya kuzaliwa."Kwa wale wanao zaliwa na maradhi hayo ni kwasababu ya upungufu wa virutubisho ambavyo mama mjamzito anatakiwa avipate kabla ya kushika mimba virutubisho hivo vinapatikana kwenye matunda,mboga za majani,mayai na vyakula vyote vyenye protini,pia maradhi ya mgongo wazi husababisha watoto kupooza na kushindwa kutumia miguu yao,"alisema

Alisema mpaka sasa kwa Mkoa wa Kagera wameshawafanyia upasuaji jumla ya watoto saba wenye vichwa vikubwa na mmoja wa mgongo wazi.Ofisa habari wa GSM Foundation Khalfani Kiwamba alisema kuwa taasisi yao iliamua kudhamini matibabu ya maradhi ya vichwa vikubwa na migongo wazi baada ya kuelezwa changamoto mbalimbali za matibabu ya maradhi hayo na uongozi wa Taasisi ya MOI.

Joviti Mchuruza akiongea kwa niaba ya wazazi ambao watoto wao wamefanyiwa upasuaji aliwashukuru timu nzima ya madaktari hao pamoja na Taasisi ya GSM kwa msaada huo wa matibabu waliowapatia wa watoto wao bure.Aliiomba jamii kuacha kuhusisha maradhi hayo na mila potofu za imani za kishirikina au mikosi kwenye familia hali inayofanya akina mama au baba kutelekezewa watoto.

Aliwaomba pia wataalam hao wasogeze huduma hiyo karibu na jamii hasa maeneo ya vijijini ambapo wapo watoto wengi wenye maradhi hayo wanateseka na hawana msaada."Nawaomba wazazi wenzangu hasa akinamama sababu sisi ndiyo tunakaa na watoto kwa muda mrefu ndiyo tunaoweza kugundua mabadiliko ya mtoto pia tusisikilize maneno ya dhihaka ya watu wa pembeni maradha haya yanatibika kabisa"alisema mzazi huyo

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu aliwashukuru madaktari pamoja na shirika la GSM Foundation kwa udhamini huo wa matibabu bure kwa watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi.Pia aliwataka wazazi wenye watoto wenye maradhi hayo wasione aibu kuwapeleka hospitali ili waweze kupatiwa matibabu bure.

Jovita Mchuruza akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)baada ya kutelekezewa watoto watano na mkewe wenye vichwa vikubwa,wanaondelea na matibabu katika hospitali ya mkoa wa Kagera.

Timu ya madaktari kutoka Taasisi ya mifupa(MOI)pamoja na wafadhili wao GSM Foundition wakiwa kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera wakimpa taarifa juu ya upasuaji wa vichwa vikubwa na mgongo wazi jwa watoto walioufanya katika Mkoa huo kwa muda wa siku tatu.Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salum Kijuu akimpa pole mmoja wa  watoto wenye maradhi ya kichwa kikubwa aliyelazwa katika hospital ya Mkoa wa Kagera baada ya kufanyiwa upasuaji na madaktari toka MOI kwa ufadhili wa Taasisi ya GSM Foundation 
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salum Kijuu akimpa pole mmoja wa  watoto wenye maradhi ya kichwa kikubwa aliyelazwa katika hospital ya Mkoa wa Kagera baada ya kufanyiwa upasuaji na madaktari toka MOI kwa ufadhili wa Taasisi ya GSM Foundation.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...