Benny Mwaipaja, WFM, Zanzibar

MAMIA ya wastaafu wa Taasisi za Muungano kutoka visiwa vya Pemba na Unguja-Zanzibar, wanaolipwa na Wizara ya Fedha na Mipango ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wamejitokeza kwa wingi kuhakikiwa huku wakiiomba Serikali iwaongezee pensheni kutokana na wengi wao kukabiliwa na hali ngumu ya maisha.

Wakizunguza katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango-Zanzibar, iliyoko katika eneo la Vuga, wastaafu hao wamepongeza hatua ya Serikali ya kuwahakiki ili kufahamu hali zao na kwamba hatua hiyo itasaidia kuwabaini watu wasio na sifa ya kupata malipo hayo kutoka Serikalini

Wastaafu Bi Sauda Ramadhani Mpambalyoto na Abuu Ali Hamisi, wameiomba Serikali iangalie namna ya kuwaongezea pensheni wataafu ambao wengi wao ni wagonjwa hawajiwezi na wengine wana afya njema, wanalima, lakini wanahitaji kuwezeshwa na Serikali ili waweze kumudu maisha ambayo wamesema yamepanda.

Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Msaidizi, Bw. Stanslaus Mpembe, amesema kuwa Wizara ya Fedha na Mipango inaendesha zoezi la kuhakiki wastaafu wanaolipwa pensheni na wizara hiyo ili kuhuisha taarifa za wastaafu kwa lengo la kupata kanzidata (database) iliyo ili kuiwezesha Serikali kuwalipa wastaafu wanaostahili.
Mkaguzi wa Ndani kutoka Wizara ya Fedha na Mipango-Bara, Bw. Paison Mwamnyasi (aliyenyoosha mkono) akitoa maelekezo kwa wastaafu wanaolipwa pensheni zao na Wizara ya Fedha na Mipango ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, waliofika katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango-Zanzibar, eneo la Vuga, kwa ajili ya uhakiki.
Zoezi la uhakiki likiwa linaendelea katika ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar, kulia ni mstaafu Bw. Amir Apacho akifanyiwa uhakiki na Mkaguzi Bi. Mary Mauki.
Mchambuzi mwandamizi wa mifumo ya kompyuta Bi. Magreth Ambrosi Akipokea namba kutoka kwa mstaafu (aliyeko dirishani) aliyopewa kwa ajili ya uhakiki. Uhakiki wa Wastaafu unafanyika katika ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango-Zanzibar, katika eneo la Vuga.
Baadhi ya wastaafu ambao ni wagonjwa wakisubiri kupata huduma wakiwa wametengewa sehemu maalumu kwa ajili ya kupata huduma hiyo ya uhakiki.
Afisa Tehama wa Wizara ya Fedha na Mipango akimfanyia uhakiki Bw Uleja Edward katika ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango-Zanzibar, zilizoko eneo la Vuga visiwani humo.
Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko-Zanzibar, Mhe. Balozi Amina Salum Ali, alipowasili katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango-Zanzibar kwa ajili ya kufanyiwa uhakiki. Aliyesimama mbele yake ni Mkaguzi wa Ndani Bw. Nicholaus Jalane.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...