Benki ya Dunia kupitia washirika wake wa Maendeleo imeamini ya kuridhika na hatua kubwa iliyochukuliwa na Jamii ya Wananchi wa Visiwa vya Zanzibar katika kusimamia miradi yao kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania{TASAF} Awamu ya Tatu katika kujiondolea Umaskini.


Viongozi wa Ujumbe wa Washirika hao wa Maendeleo ulitoa kauli hiyo wakati ukitoa tathmini ndogo kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar baada ya kumaliza ziara yake ya kukagua miradi ya Jamii inayotekelezwa kupitia Tasaf Tatu katika maeneo mbali mbali ya Mjini na Vijijini Unguja na Pemba.

Kiongozi wa Ujumbe huo kutoka Benki ya Dunia Bwana Moderes Abdulah alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba ziara ya Ujumbe wake imeshuhudia maendeleo makubwa yaliyopatikana katika Jamii kutokana na kundi kubwa la Wananchi lilivyoamua kutekeleza kwa ufanisi mkubwa miradi yao waliyoianzisha. 

Bwana Moderes alisema Zanzibar imeonyesha mfano bora katika uendelezaji wa miradi ya Maendeleo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania {TASAF} awamu ya Tatu kiasi kwamba Uongozi wa Benki ya Dunia kupitia Washirika wake imefurahia hatua hiyo ya mafanikio.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Mwakilishi wa Benki ya Dunia Bwana Moderes Abdula aliyeuongoza Ujumbe wa Washirika wa Maendeleo ulikuwepo Zanzibar kwa siku Nne kukagua miradi ya Tasaf Awamu ya Tatu. Kati kati yao ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania Bwana Ladislas Mwamanga.
Balozi Seif akizungumza na Ujumbe wa Benki ya Dunia ulioambatana na washirika wa Maendeleo hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar uliofika kukagua miradi ya Tasaf.
Balozi Seif kati kati waliokaa vitini akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Viongozi wa Benki ya Dunia na washirika wake wa maendeleo mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.  Kushoto ya Balozi Seif ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mihayo Juma Nhunga, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Nd. Joseph Abdulla Meza na Bibi Azzah Ammin kutoka Shirika la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA).  Kushoto ya Balozi Seif ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Jamii Tanzania (TASAF) Nd. Ladislas Mwamanga, Mwakilishi wa Benki ya Dunia Bwana Moderes Abdula na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Ahmad Kassim Haji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...