Na Mathias Canal, Dar es salaam

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori Leo Mei 26, 2017 ameiagiza Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo inayoongozwa na Ndg John Lipesi Kayombo kuanza haraka ujenzi wa Shule ya Sekondari kwa ajili ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam.

Agizo hilo amelitoa wakati akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya Msingi Mvurunza mara baada ya kufanya ziara ya kikazi katika Kata hiyo ili kujionea hali ya maendeleo ya elimu sambamba na kubaini changamoto zinazowakabili wananchi katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Ubungo na hatimaye kuzitatua.

Katika ziara hiyo ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo imehudhuriwa pia na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo, Afisa Tarafa ya Kibamba, Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Ubungo, Diwani wa Kata ya Kimara, Mtendaji Kata ya Kimara, Wenyeviti na Watendaji wa Mitaa sambamba na Baadhi ya Wananchi wa eneo hilo.

Agizo la Mkuu wa Wilaya ya Ubungo linakuja zikiwa ni siku chache zimepita tangu kutoa maagizo kama hayo katika Shule ya Msingi Ubungo Plaza, Shule ya Msingi Kawawa na Shule ya Sekondari Mburahati ambapo kote huko ameelekeza kuanza haraka ujenzi wa Madarasa sambamba na Vyoo kwa ajili ya wanafunzi na walimu.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori (Kulia), Diwani wa Kata ya Kimara Mhe Manota wakikagua eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Sekondari ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akikagua ukarabati wa Zahanati ya Mavurunza mara baada ya kuzuru kukagua eneo litakalojengwa Shule ya Sekondari ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017 ambapo ameahidi kusaidia kukamilika haraka kwa ujenzi huo.
 Hali ya ukarabati wa Zahanati ya Mavurunza iliyopo katika Mtaa wa Mavurunza Kata ya KImara
Diwani wa Kata ya Kimara Mhe Manota akimuongoza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori kukagua ukarabati wa Zahanati ya Mavurunza mara baada ya kuzuru kukagua eneo hilo. Leo Mei 26, 2017 ambapo ameahidi kusaidia kukamilika haraka kwa ujenzi huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...