Na. Immaculate Makilika- MAELEZO

 Mtafiti wa masuala ya Uchumi na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam  Dkt.Haji Semboja anasema kuwa amefurahishwa na ripoti ya Kamati Maalum iliyoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  John Pombe Magufuli  ya  kuchunguza mchanga wa madini kwenye makontena 277 yaliyozuiwa na serikali kusafirishwa kwenda nje kwaajili ya uchenjuaji.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam  katika mahojiano na mwandishi wa habari hii, Dkt.Semboja alisema kuwa, hatua hiyo ni nzuri na ya kuridhisha  kwa vile Rais Magufuli amefanyia kazi suala hilo ambalo limekua likizungumzwa kwa muda mrefu na baadhi ya wasomi,wanaharakati na hata wanasiasa hapa nchini.

“Mimi ni kati ya Watanzania waliofurahishwa na maamuzi ya Rais, nina furaha kubwa hasa ukizingatia niliwahi kushiriki katika uandaaji wa sera za madini na uwekezaji, na ni wazi kuwa tumekuwa tukiibiwa kwa kiwango kikubwa katika sekta ya madini” alisema  Dkt.Semboja.

Malalamiko haya  ya wizi na utoroshaji wa madini yamekuwepo kwa muda mrefu,  kitu ambacho tulikua tukizungumza    sasa  kimethibitishwa , baada ya Rais Magufuli  kupokea ripoti hiyo ya mchanga”, aliongeza Dkt.Semboja.

Aidha, Dkt.Semboja amemshauri  Rais Magufuli  kuendelea kuwatumia wataalamu mbalimbali waliopo nchini na kuiomba Serikali iwe na utaratibu wa kuwatumia watu wake ambao wengi ni wazalendo na wana uchungu na nchi yao.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Rais Dkt John Pombe Magufuli

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...