Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, inawashikilia watu wanne wakiwemo wahudumu wawili wa chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Mwananyamala kwa kosa la kupasua maiti na kuiba dawa za kulevya kisha kwenda kuziuza.

Kamanda wa kanda Maalum, Kamishna Simon Sirro amesema, mbali na wahudumu hao wa chumba cha kuhifadhia maiti, mtuhumiwa mwingine ni Ally Mahamud Nyundo (41) ambaye ni miongoni mwa watu waliotajwa katika orodha ya Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kujihusisha na biashara hiyo.

“Watuhumiwa walikamatwa kutokana na kuwepo taarifa ya kupokelewa kwa mwili wa raia wa Ghana katika hospitali hiyo, aliyedaiwa kufariki katika nyumba ya kulala wageni kutokana na kumeza dawa za kulevya,” amesema Kamanda Sirro.

Amesema mtu huyo ambaye bado hajafahamika jina lake alifariki dunia Machi 14 mwaka huu katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Red Carpet iliyoko Sinza, wilaya ya kinondoni.

Kamanda Sirro amewataja waliokamatwa kuwa ni Omari Rukola (47) na Athuman Mgonja (48) wote wahudumu wa chumba cha kuhifadhia maiti na katika mahojiano walikiri kuuchana mwili wa marehemu na kuchukua kete 32 za dawa za kulevya ambapo alimkabidhi Omary Wagile (47) mfanyabiashara ambaye naye aliziuza kwa Nyundo.

Kamanda Sirro amesema watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa na baada ya uchunguzi kukamilika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...