THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


There was an error in this gadget

Bi. Bernadette Mathias akiimba Wimbo wa Tanzania Nakupenda kwa Kiswahili katika sherehe za kumtunuku JK shahada ya heshima chuo kikuu ya newcastle, australia

Bi. Bernadette Mathias ambaye kwa kushirikiana na mpiga piano mumewe Profesa Philip Mathias wakitumbuiza kwa wimbo wa "Tanzania, Tanzania nakupenda kwa moyo wote" kwa ufasaha na kusisimua waliohudhuria sherehe za Rais Jakaya Mrisho Kikwete kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Chuo Kikuu cha Newcastle nchini Australia Julai 29, 2015. 


Introducing Imperial Solutions for all your car needsBINTI YETU ANENA BAADA YA KUSHINDWA KUPATA KURA ZA KUTOSHA TABORA

Baada ya kura kutotosha kumfanya apite katika kura za maoni kugombea Ubunge kwa viti vya Vijana mkoani Tabora, Zahara Muhidin Issa Michuzi (pichani) amepokea matokeo kwa moyo mkunjufu na kumpongeza mshindi Irene Uwoya na kumuahidi ushirikiano katika mambo yote mema ya kuendeleza vijana mkoani humo.
Zahara ambaye sasa ataelekeza nguvu zake katika kusaka digrii ya pili ya uchumi, amesema kwamba anawashukuru wajumbe wa mkutano wa uchaguzi, baba yake, mama walezi, kaka Mkala Fundikira wa Tanzania Bloggers Network (TBN) kanda ya Magharibi na wana TBN wote wa ndani na nje ya nchi akiwemo kaka Jeff Msangi wa Canada na Mubelwa Bandio na DJ Luke wa Marekani, wanahabari wote wa makundi ya Whatsapp chini ya Francis Godwin na walimu wake pamoja  na wananchi wote kwa ujumla kwa kumpa heshima ya kumuunga mkono kwa kujitokeza kujaribu kuomba nafasi hiyo.
Amesema kushindwa kwake hakumaanishi lolote zaidi ya kwamba demokrasia imechukua mkondo wake na aliyehitajika kuendeleza mapambano amepita na yeye hana kinyongo naye na ataendelea kuutumikia mkoa wa Tabora  katika nafasi yake ya mtu ambaye si kiongozi.
Zahara ametoa mwito kwa wagombea wa nafasi zote kwamba kushindwa ni moja ya matokeo katika ushindani wowote hivyo ipo haja ya kujenga utamaduni wa kukubali matokeo bila ya hasira ama kinyongo kwani dunia i duara, na kwamba mlango mmoja ukifungwa kuna mwingine utafunguka.
Amesema hana mpango wa kuhama CCM ambayo anaiamini kuwa ni chama ambacho kitaenzi na kutunza hadhi na mustakabali wa Taifa la Tanzania kuliko chama chochote.
"Kushindwa kwangu kupata kura za kutosha sio mwisho wa dunia. Nina imani kwamba wapiga kura walijua wanachokifanya. Mimi ni nani kuwaoneshea kidole?  Maisha yaendelee kama kawaida na Mola awajaalie wote kwa yote" alisema.


MGOMBEA MTEULE WA URAIS CCM,DKT MAGUFULI KUCHUKUA FOMU TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI LEO JUMANNE

 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akifafanua jambo kwa umakini mbele ya waandishi wa habari  kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. 
  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. 

 Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.

 MGOMBEA mteule wa urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Pombe Magufuli, leo Jumanne Agosti 4, 2015  atawasili Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kuchukua fomu ya kuomba kugombea Urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba Mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema, msafara wa Dk. Magufuli  kwenda kuchukua fomu hiyo, utaanza saa tano asubuhi ukitokea Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam.
Nape amesema, msafara ambao utaambatana na shamrashamra za aina yake, utapita katika Barabara za Morogoro, Bibi Titi Mohammed na Ohio kabla ya kufika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi zilizopo Posta House, karibu na makao Makuu ya Jeshila Polisi.
Amesema, Dk. Magufuli ambaye ataambatana na Mgombeamwenza wake, Mhe. Samia Suluhu, mbali na makada, wapenzi na wanachama wa CCM,atasindikizwa na viongozi mbaimbali wakiwemo, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Dk. Magufuli alichaguliwa na Mkutano  Mku wa CCM uliofanyika Oktoba 11, 2015, mjini Dodoma, baada ya kuwashinda wagombea wenzake, Dk. Asha-Rose Migiro na Balozi Amina Salum Ally. 


TASWIRA MBALI MBALI ZA MAONYESHO YA NANE NANE MKOANI LINDI

Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa wilaya ya Lindi na Kilwa Mwal. Mariam R. Mtima (wa kwanza kushoto) akimsikiza Afisa Masoko na Uhusiano wa Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundo Mbinu (UTTPID) Kilave Atenaka (wa pili kulia) wakati mkuu huyo wa wilaya alipotembelea banda la taasisi hiyo leo katika viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi. Kauli mbiu ya Manesho ya Nane Nane mwaka huu ni “Matokeo Mkubwa Sasa, Tuchague Viongozi Bora kwa Maendeleo ya Kilimo na Ufugaji”.
Afisa Maendeleo ya Jamii wilaya ya Masasi (kushoto) akimsikiliza Mhasibu kutoka Idara ya Pensheni Wizara ya Fedha Imelda Mzatulla (katikati) wakati wa Manesho ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi ambayo yanaongozwa na kauli mbiu “Matokeo Mkubwa Sasa, Tuchague Viongozi Bora kwa Maendeleo ya Kilimo na Ufugaji”. Wa kwanza kulia ni Mchumi kutoka Idara ya Bajeti ya Serikali Wizara ya Fedha Prosper Fivawo.
Afisa wa hali ya Hewa kutoka Pemba Suleiman Ali Juma akiwafafanulia wanafunzi kutoka shule ya Masingi Tulieni kata ya Mnazi Mmoja Mkoani Lindi namna mamlaka ya hewa inavyofanya kazi zake kwa manufaa ya Wanzania kujua masuala ya hali ya hewa kila siku. Wwakati mkuu huyo wa wilaya alipotembelea banda la taasisi hiyo leo katika viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi. Kauli mbiu ya Manesho ya Nane Nane mwaka huu ni “Matokeo Mkubwa Sasa, Tuchague Viongozi Bora kwa Maendeleo ya Kilimo na Ufugaji”.


Mwili wa marehemu mzee Francis Kitime wasafirishwa kwa mazishi

Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wa familia ya marehemu Mzee Francis Raphael Kitime wakiwa katika ibada ya kumuombea jana jijini Dar es Salaam. Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wa familia ya marehemu Mzee Francis Raphael Kitime wakiwa katika ibada ya kumuombea jana jijini Dar es Salaam.Padre wa Kanisa Katoliki Parokia ya Huruma ya Wagonjwa Muhimbili akizunguka kulibariki jeneza lenye mwili wa Marehemu Mzee Francis Raphael Kitime kwenye ibada ya kumuombea iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana kabla ya kusafirishwa kwenda Iringa kwa Mazishi. Padre wa Kanisa Katoliki Parokia ya Huruma ya Wagonjwa Muhimbili akizunguka kulibariki jeneza lenye mwili wa Marehemu Mzee Francis Raphael Kitime kwenye ibada ya kumuombea iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana kabla ya kusafirishwa kwenda Iringa kwa Mazishi.Familia ya marehemu Mzee Francis Raphael Kitime (mbele) wakiwa kwenye ibada ya kumuombea marehemu. Familia ya marehemu Mzee Francis Raphael Kitime (mbele) wakiwa kwenye ibada ya kumuombea marehemu.Mwanamuziki mkongwe na nguli nchini Tanzania, John Kitime ambaye ni mtoto wa marehemu Mzee Francis Raphael Kitime akitoa historia fupia ya marehemu baba yake mara baada ya ibada. Mwanamuziki mkongwe na nguli nchini Tanzania, John Kitime ambaye ni mtoto wa marehemu Mzee Francis Raphael Kitime akitoa historia fupia ya marehemu baba yake mara baada ya ibada. 

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI


mdau cosato david chumi aibuka kidedea kura za maoni

 Mdau mkubwa wa Globu ya Jamii Cosato David Chumi ambaye ni afisa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akielekea jukwaani kuwashukuru wapiga kura wake baada ya kuibuka kidedea katika kura za maoni katika kugombea Ubunge jimbo jipya la Mafinga mjini mkoani Iringa kwenye hafla iliyofanyika katika uwanja wa Changarawe.  Jimbo hilo limemegwea kutoka iliyokuwa Mufindi Kaskazini na kata moja ya Bumilayinga toka Mufindi Kusini na kuwa Mafinga mjini
 Mdau mkubwa wa Globu ya Jamii Cosato David Chumi akimwaga sera na kushukuru wapiga kura wake
Matokeo rasmi katika kura za maoni Mafinga mjini


JK aaga wananchi Tanga, afungua wiki ya nenda kwa usalama barabarani


.Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia mamia ya wakazi wa mji wa Tanga waliojitokeza katika mkutano mkubwa wa hadhara ambapo aliwaaga rasmi na kumpa zawadi mbalimbali jana  jioni 

 Baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali za mkoa wa Tanga wakiandamana wakati wa sherehe za maadhimisho  ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani yaliyofanyika kitaifa katika viwanja vya Tangamano jijini Tanga
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizindua stika maalumu zing’aazo zitakazosaidia kupunguza ajali kwakuwa magari makubwa yataonekana kwa mbali na waendesha gari wengine hivyo kuepisha magari kugongana.kulia ni Kamanda Mkuu wa Usalma Barabarani kitaifa Mohamed Mpinga.
 Askari wa kikosi cha usalama barabarani akimuonesha Rais Kikwete kidhibiti mwendo cha magari maarufu kama tochi wakati Rais liapotembelea mabanda ya maonyesho wakati wa wiki ya usalama barabarani ilkiyofanyika kitaifa mkoani Tanga
Mtoto wa shule ya msingi mjini Tanga Doreen John akitoa maelezo ya matumizi sahihi ya barabara kwa Rais Dkt,Jakaya Mrisho Kikwete wakati Rais alipotembelea mabanda kadhaa ya maonyesho katika viwanja vya Tangamano,mjini Tanga wakati wa maadhimisho ya sherehe ya wiki ya nenda kwa usalama iliyofanyika mkoani Tanga.Picha na Freddy Maro


MAKALA YA SHERIA: IJUE NAMNA YA KUPATA MSAMAHA WA KODI NA USHURU BANDARINI.

Na Bashir Yakub
Sheria  ya  Uwekezaji  ya  Mwaka  1977 imehamasisha  uwekezaji  kwa  wazawa  na  wasio  wazawa  kwa  kuweka  mazingira  rafiki  kwa  wajasiriamali katika  nyanja  zote.  Wapo  ambao  wanajua fursa hizi  na wamezitumia   kujipatia  maendeleo  na  wapo  ambao  hawajatumia  fursa  hizi.  Nataka  niseme  kitu  kimoja  kuwa  wazawa  wengi  wameshindwa  kufanikiwa  kwa  kutojua  uwepo wa fursa. Wengi  wangependa  kutumia  fursa   kama  zipo  lakini  hawajui ziko  wapi na  zinapatikana vipi.
Badala  yake  wageni  na  watu  wengine  ambao  si  wenye  asili  halisi  ya  Tanzania  ndio  wamekuwa  wakihabarishana  kuhusu  fursa  hizi  wanazitumia  na  wanafanikiwa sana.  Wenyeji  halisi   wa  nchi  hii  wanabaki  kutazama  mafanikio  ya  watu  hawa  wasijue  yanapatikanaje. 
Ziko  fursa  ambazo  zimetolewa  na  serikali  na  kuainishwa  na  sheria  mbalimbali  mojawapo  ikiwa  hii  ya  kusamehewa  kodi  kwa bidhaa  zinazoingizwa  nchini  kutoka  nje  ya  nchi. 
Wafanyabiashara  watakubaliana  na  mimi  kuwa  ikiwa  utapata  msamaha mzuri  wa  kodi bandarini  basi  unayo  nafasi  kubwa  ya  kutengeneza  faida  kubwa  katika  biashara  yoyote  utakayoamua  kufanya.

Mara  zote  kodi  ndio  huwa  tatizo. Makala  haya yataeleza  namna  ya  kupata  msamaha  wa  kodi. Kusoma zaidi BOFYA HAPA


wapiga kura wampongeza jerry silaa kwa kushinda katika kura za maoni jimbo la ukonga

 Wananchi wa Jimbo la Ukonga wakiwa nyumbani kwa mgombea ubunge wa jimbo hilo aliyeibuka kidedea, Jerry Silaa.
Mgombea Jerry Silaa akishukuru wapiga kura baada ya kuibuka kidedea kwa kupata kura 10,382 huku mshindani wake PATEL Ramesh akipata kura 7355. 
Mgombea ubunge huyo aliwashukuru wananchi na wanaCCM waliokwenda nyumbani kumpongeza na kuwapongeza wagombea wenzake wote,na kuongeza kuwa wiki moja waliyokuwa pamoja amejifunza mengi, anaamini watashirikiana kufanikisha Ushindi wa CCM October 25.


FFU-Ughaibuni wafanya kweli Liga Summer Festival 2015

 Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band maarufu kama
FFU ughaibuni ukipenda waite viumbe wa ajabu Anunnaki Alien juzi wikiendi walifanikiwa kuwadatisha washabiki wa muziki nchini Latvia katika maonyesho ya Summer Festival,yaliyofanyika Liga. 
Bendi hiyo yenye makao yake nchini Ujerumani inayoongozwa na mwanamuziki mahiri Ebrahim Makunja aka  Kamanda Ras Makunja,imejizolea umaarufu wa kimataifa kwa kutumia mdundo wake wa "Bongo Dansi" uliochanganywa na rumba la kukata na shoka mdundo huo umefanikiwa kuwazoa na kuwadatisha akili washabiki wengi wa kimataifa.
Ngoma Africa Band kwa sasa wanatamba na single CD yao mpya 'La Mgambo"
yenye mbili za kumuaga Rais JK.
Unaweza kuwasikiliza at www.reverbnation.com/ngomaafricaband au uungana nao at www.facebook.com/ngomaafricaband
 Gwaride limenoga Latvia katika maonyesho ya Summer Festival,yaliyofanyika Liga. 
 Mashabiki wa Latvia katika maonyesho ya Summer Festival,yaliyofanyika Liga. 
 Mambo ya Latvia katika maonyesho ya Summer Festival,yaliyofanyika Liga. 


Bwana Apewe Sifa na Kuinuliwa

Wapendwa Watanzania na marafiki popote pale duniani,

Kwa niaba ya uongozi wa Tanzania Global Prayer Movement (TGPM) natoa shukrani za dhati kwa wale wote waliojiunga nasi kwenye maombi ya Jumapili hii na siku zote kuanzia Jumapili July 26 tukiombea utakaso wa kiti cha Raisi, Ikulu, viti vya wabunge na madiwani pamoja na amani wakati vyama vinajipanga sawa sawa na uchaguzi.

Yafuatayo ndiyo tunayoendelea kuombea mpaka siku ya Jumapili Agosti 9 ambapo itakuwa hitimisho la wiki tatu kuombea haya maswala. Endelea kuinua jina la Bwana.

1)   Omba Mungu akupe mzigo wa kuombea nchi yako ya Tanzania.
2)   Ombea amani nchini wakati vyama vinakamilisha uchaguzi wa wagombea wao wa nafasi ya Raisi.
3)   Ombea utakaso wa Kiti cha Uraisi wa Tanzania.
4)   Ombea utakaso wa Ikulu ikiwa ni mahali anapofanyia kazi Raisi wa Tanzania, pamoja na ikulu ndogo mikoani.
5)   Ombea utakaso wa viti vya wabunge na madiwani nchi nzima.
6)   Ombea mgombea Uraisi wa UKAWA kama jina litakuwa limetoka. Kama bado, tutaendelea kuombea amani huku mchakachuo ukiendelea.


Please join us via a prayer conference call this Sunday. To join the conference call every Sunday, please dial (218) 895 9661 and passcode is 222555.  The prayer starts at 9pm Eastern, 8pm central, 7pm Mountain or 6pm Pacific time.

For more information about Tanzania Global Prayer Movement (TGPM), please visit our website at:


bendera ya tanzania yatamba katika tamasha la afrifest marekani

Na Profesa Mbele
Jana, tarehe 1 Agosti, tamasha la Afrifest lilifanyika mjini Brooklyn Park, Minnesota. 
Hili ni tamasha ambalo huandaliwa mara moja kwa mwaka na bodi ya Afrifest Foundation ambayo mimi ni mwenyekiti wake. ili kuwakutanisha wa-Afrika, watu wenye asili ya Afrika waishio Marekani ya Kaskazini, Kati, na Kusini, pamoja na Caribbean, na pia watu wa mataifa mengine. Lengo kubwa ni kufahamiana, kuelimisha, na kuuenzi mchango wa watu weusi duniani kote, katika nyanja mbali mbali. 

Hiyo jana ilikuwa ni mara ya kwanza kwa bendera ya Tanzania kupepea kwenye tamasha la Afrifest. Baada ya kushiriki matamasha na kujionea wenzetu wanavyotumia fursa kuzitangaza nchi zao, nilijiuliza kwa nini nisitafute bendera ya Tanzania, kama nilivyoeleza katika blogu hii.

Hatimaye, nilifanya uamuzi wa kununua bendera, niwe ninaipeperusha kwenye matamasha ninayoshiriki, maadam fursa zipo. Hapo kushoto naonekana na binti zangu Assumpta na Zawadi kwenye meza yetu, hiyo jana.

Kusoma zaidi BOFYA HAPA


Binti yetu Zahara kura hazikutosha dhidi ya Irene Uwoya Tabora


Zahara Muhidin Michuzi akiwa nje ya ukumbi wa uchaguzi mapema leo.
Na Mkala Fundikira wa 
TBN kanda ya Magharibi
Leo hii mchana binti ya mpiga picha na blogger maarufu nchini Muhidin Issa Michuzi Bi Zahara Michuzi alishindwa kupata kura za kutosha kumwezesha kushinda nafasi ya ubunge wa vijana kupitia tiketi ya CCM mkoa wa Tabora baada ya msanii wa filamu Bi Irene Uwoya kupata kura 34 kati ya 39 zilizopigwa.

Zahara ambaye ni mhitimu wa shahada ya uchumi toka chuo kikuu cha UDOM aliyakubali matokeo hayo bila kinyongo  na kusema :
"Napenda kuwashukuru wagombea wenzangu na wajumbe wote. Pamoja na kura mlizonipigia hazikutosha leo lakini nitabaki na azma yangu ya kuwatumikia wana Tabora" wajumbe walimshangilia sana na kumpongeza kwa ukomavu wa kisiasa aliouonesha kwani mgombea  mwenzie Mariam Shamte alisusia na kuondoka ukumbini. 
Mariam alimteua nduguye Hapsa kumwakilisha ktk uhesabuji kura hizo ambazo yeye Mariam alipata kura 3. Hakuingia ukumbini katika usomwaji wa matokeo.

Awali mgeni rasmi wa mkitano huo mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Bw Hassan Wakasuvi aliwaeleza wajumbe kuwa Obama alizaliwa na baba raia wa Kenya na mama Mmarekani lakini leo hii anaiongoza Marekani, hivyo wasione ajabu kama pana mgombea asiyetokea Tabora kiasilia. 
Bila shaka alikuwa akimzungumzia Irene Uwoya ambaye kabla ya uchaguzi wakazi wengi wa Tabora walielekea kutomkubali kwa kusema kwa nini CCM ituletee mgombea toka Arusha, Moshi au Dar es Salaam, na kwa nini Irene asigombee Dar anapoishi au Kwao kaskazini? kwani Tabora hakuna vijana wenye uwezo wa kugombea? 
Waliendelea kuhoji kuwa ni vipi Irene atayajua matatizo ya vijana wa Tabora ambao hawajui wala hana uelewa na mkoa huo? 
Lakini hayawi hayawi hatimaye yamekuwa kwa Irene ameibuka mshindi katika kinyang'anyiro hicho. 
Kama maneno ya Mwenyekiti huyo wa CCM mkoa wa Tabora yalifanya kazi kusababisha Irene Uwoya achaguliwe kwa kishindo mimi na wewe hatujui.
Zahara Michuzi akiwa na wagombea wenzie Mariam katikati na Irene kulia
Irene Uwoya mcheza sinema maarufu nchini alishinda uchaguzi huo kwa kura 34 kati ya 39 zilizopigwa.
Mariam Shamte alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 3
Zahara Muhidin Michuzi alishika nafasi ya 3 kwa kupata kura 2 katika kura 39 zilizopigwa.
Bi Mariam Amir katibu wa UVCCM mkoa wa Tabora akisoma tamko la kuunga mkono na kupongeza kuchaguliwa Bw John Magufuli kuwa mgombea urais wa Jamhuhuri ya muungano wa Tanzania.
Katibu mkuu wa CCM mkoa wa Tabora Bibi Janeth Kayanda akisalimia wajumbe leo hii mapema.
Mwenyekiti mstaafu UVCCM wilaya ya Tabora mjini Nassor Wazambi akifuatilia mchakato.
Wagombea wakiwasalimia wajumbe wa mkutano maalumu leo mapema.
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Tabora Bw Seif Gulama (Kazuge) akitoa yake machache.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Mzee Hassan Wakasuvi akihutubia mkutano huo.
Sunday Kabaye akiwa amebeba sanduku la kura mara baada ya kura hizo kuhesabiwa nyuma akifuatiwa na Irene Uwoya na Zahara Michuzi.
Irene Uwoya akitokwa machozi kabla ya kutangazwa mshindi
Kada wa CCM Jaha Kaducha kushoto akiwa na Mwalimu Nassoro Wazambi.
Msimamizi wa uchaguzi Bw Mwambeleko akisoma matokeo ya uchguzi huo leo mchana mijini Tabora
Team Irene wakifuatilia mchakato


introducing bona productions

KWA KIPINDI CHA MIAKA MITANO TUMEKUWA TUNA VIDEO MOVIES, CONFERENCE NA DOCUMENTARY, SASA TUNAPANUA BIASHARA MPAKA KWENYE SHEREHE.
KWA MAHITAJI YAKO YA VIDEO SHOOTING YA HARUSI, SEND-OFF, KITCHEN PARTY, GRADUATION, WASILIANA NASI, TEL - NOELA 0715 432 310
KARIBUNI SANA.


SIO JAMBO LA AJABU KWA MWANACHAMA YEYOTE KUHAMA CCM-NAPE


M-PAWA KUWAFIKIA WANANCHI POPOTE WALIPO MTAANI

Baadhi ya Mabalozi wa Vodacom Tanzania wanaoenda kutoa elimu kwa wateja wa kampuni hiyo na wananchi kwa ujumla kuhusiana na huduma ya M-Pawa wakimsikiliza Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa kampuni hiyo,Kelvin Twissa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘M-Pawa Tumekufikia’ yenye lengo la kuwaelimisha wateja wake nchi nzima kuhusiana na manufaa ya huduma ya M Pawa inayowawezesha kujiwekea akiba na kujipatia mikopo nafuu kwa urahisi zaidi.Uzinduzi huo ulifanyika makao makuu ya kampuni hiyo Mlimani City jijini Dar e Salaam leo.
Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa Vodacom Tanzania,Kelvin Twissa(wakwanza kushoto)na Ofisa Mkuu wa Idara ya M-Pesa,Jacques Voogt wakizindua kampeni ya ‘M-Pawa Tumekufikia’ yenye lengo la kuwaelimisha wateja wake nchi nzima kuhusiana na manufaa ya huduma ya M Pawa inayowawezesha kujiwekea akiba na kujipatia mikopo nafuu kwa urahisi zaidi.Uzinduzi huo ulifanyika makao makuu ya kampuni hiyo Mlimani City jijini Dar e Salaam leo.

Wateja wa Vodacom Tanzania na wananchi kwa ujumla wanaonufaika na huduma ya M-Pawa inayotolewa na kampuni hiyo kwa kushirikiana na benki ya CBA itawafikia watanzania wengi zaidi baada ya kampuni hiyo kuzindua kampeni ya kabambe ya ‘M-Pawa Tumekufikia’ yenye lengo la kuwaelimisha wateja wake kuhusiana na faida na jinsi ya kunufaika na huduma hii inayowawezesha kujiwekea akiba na kujipatia mikopo nafuu kwa urahisi zaidi.

Kampeni ya M-Pawa tumekufikia ambayo imezinduliwa leo jijini Dar es Saaam itafanyika nchini nzima ambapo wataalamu wa huduma watapita kila mkoa kutoa elimu juu ya matumizi na manufaa yake kwa ajili ya kujikwamua kimaisha. Wanachi wanaoishi mijini na vijijini watapata fursa ya kuelimishwa kuhusu M-Pawa na huduma nyingine za Vodacom Tanzania. Mbali na elimu, wateja watajipatia zawadi mbalimbali na kupata burudani kabambe kutoka kwa wasanii nguli wa hapa nchini.