Maaskofu na wachungaji wa makanisa ya kipentekosti wakiingia ukumbini katika Hoteli ya Tamari iliyopo Mwenge tayari kwa kutoa tamko lao.
Katibu wa Maaskofu wa makanisa ya Kipentekosti Dk. Damas Mukassa akisoma tamko la maaskofu hao Dar es Salaam jana, kuhusu sakata la kukamatwa kwa Askofu wa Kanisa la Uzima na Ufufuo, Josephat Gwajima ambalo leo hii wanatarajia kwenda kumuona Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Mangu kuzungumzia suala hilo. Kulia ni Askofu Dk.Mgullu Kilimba na Askofu Mwaviga Mwafululila.
 Askofu Dk. Paul Shemsanga akizungumza katika mkutano huo ambapo maaskofu hao walitoa tamko lao.

BOFYA HAPA KUSOMA HABARI KAMILI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. "Mtu mzima" haombewi msamaha, bali anaomba msamaha mwenyewe, anatubu na kuahidi kamwe hatarudia tena.

    ReplyDelete
  2. hawa wachungaji ni vichaa au nini? wanaandamana kumwombea msamaha wakati mwenyewe Gwajima anasema alikuwa anafanya kazi yake, sasa na sisi waumini wa kikatoliki tutaandamana hadi polisi ili tujue undani wake wa kumtukana kiongozi, hawa wachungaji wa pentecostal kama wamechanganyikiwa kudhulumu watu, mtaona kwa Mungu

    ReplyDelete
  3. Unampelekeaje bastora marehemu? atajikinga hali amekufa? kweli ni kichekesho hicho. Acheni sheria ya serikali ichukue mkondo wake, msilete habari ya kusema serikali haifanyi haki kumchukulia hatua askofu wenu. Kwa nini alipokuwa anamtukana Askofu Pengo hamkuandamana kwenda kumpa pole Pengo ya matusi makubwa aliyotoa Gwajima? na mbona hamkumshauri Gwajima kwenda kumwomba msamaha Pengo kama muliona kakosea? acheni fujo kabisa ninyi ndo munaleta mvurugano nchini.

    ReplyDelete
  4. Jamani huyo mtu c yuko kwenye mikono ya sheria, sasa nini tena msiosubiri sheria ifuate mkondo wake! au ndo mnataka kuwaonesha waumini wa dini nyengeni nyinyi ndo mnaoiongoza dola?

    ReplyDelete
  5. Hawa madaktari kweli au kanyabwoya? Kwanini madaktari hawajui sheria kiasi cha kutaka kuingilia mwenendo wa makosa ya jinai? Kama kuomba msamaha dili basi wamwombe Mungu wao wanayemchuuza aachiwe tapeli mwenzao.

    ReplyDelete
  6. Inasikitisha sana kwa watu wanaojiita wa kiroho kutaka kutetea uozo wa mwenzao. Matusi aliomtukana Mwadhama Askofu Pengo ni matusi ya yaliyolidhalilisha hata kanisa zima. Haiingii akilini kiongozi wa kiroho kutukana na kuropoka maneno ya ya matusi na kejehi kwa kiongozi mkubwa huyo. Kama angekuwa na akili timamu huyo gwajima angemfuata Askofu Pengo akaongea naye kiroho na kiutumishi.

    Mimi najiuliza hawa wanaojiita maaskofu wa kipetekoste hivi wanaupateje uaskofu huo maana sielewi kila anaibuka amevuna wakristo kanisa mwake tayari anajivika kofia ya uaskofu. Hiyo nafasi imejinasiwa sana na hawa watumishi wa kipentekoste. Kama kweli angekuwa askofu kwa ngazi hiyo angefanya ujinga huo?? Wamejitundika mavazi ya kizambarau kujiita maaskofu ili wapate heshima kwa watu halafu wanaenda kudhalilisha viongozi kwa kutukana matuzi ovyoovyo kwenye majukwaa ya mahubiri yao. Watamuombeaje msamaha mtu ambaye yuko hai ana akili timamu na anasema alikuwa kwenye kazi yake ya kukemea upotoshaji.Hivi aliendaje kuhojiwa na hali akijua anaumwa kichwa??

    ReplyDelete
  7. Huyu ngwajima inabidi aombe msamaha mwenyewe hata Kama askofu mkuu Pengo amemsamehe. Sasa wewe ulijigamba kutukana upo unahangaika hospitalini sasa. Pole sana ngwajima ila nadhani hutarudia tens umepata fundisho

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...