WAJUMBE wa Sekreatrieti ya Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya (NEC) ya CCM, jana walitembelea maeneno yaliyofikwa na mafuriko ya Mkoa wa Mjini Magharibi kwa lengo la kuangalia na kuwafariji wananchi walioathirika na mkasa huo.


Wakiongozwa na Mwenyekiti wao, ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Vuai Ali Vuai, wajumbe hao wa Sekreatrieti walitembelea maeneo mbali mbali mkoani humo ikiwemo Mpendae kwa Binti Amrani, Tomondo na Mwanakwerekwe, ambayo yalikumbwa na kadhia hiyo.
Walitumia nafasi hiyo kuwafariji baadhi ya wananchi waliathirika na mafuriko hayo, ambapo baadhi nyumba zimejaa maji na nyengine kuanguka kuta zake, na kusabababisha hasara kubwa.

Wajumbe hao wamewataka wale wote waliokumbwa na janga hilo, kuwa na moyo wa subra na kuiachia Serikali kupitia kitengo cha maafa kutafakari na kuona nini la kufanya. Aidha, wametoa wito na haja kwa jamii nzima ya Wazanzibari kuchukua tahadhari hasa wakati huu wa mvua za masika zinazoendelea kunyesha.

Mvua hiyo kubwa iliyonyesha kwa muda wa masaa matatu mfululizo, kuanzia saa 3:30, iliwafanya wananchi wa Manispaa ya Zanzibar na vVitongoji vyake kushindwa kutekeleza shughuli zao za kimaendeleo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 06, 2015

    Waathiriwa wa mvua poleni, halmashauri ya Zanzibar na idara nyngine husika maji ya kipungua kazi yenu ya kushughulikia mitaro na njia za mvua na kuinua kwa vifusi sehemu zingine ndiyo itaanza ili tatizo hili lisijirudie.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 06, 2015

    Hiyo picha ya hapojuu hilo ni dampo au nini?

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 06, 2015

    Jamani, kumbe hali ndo mbaya hivyo? lo! poleni sana ndugu zetu wa Zanzibar. Mola awape utulivu na amani ili murudi katika hali yenu ya kawaida.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 07, 2015

    ndugu zangu wakati umefika kuikumbuka ile nyimbo ya zamani
    "mapinduzi ya unguja hakika yana maana". Miaka yote hii bado nchi haina mfumo maridhawa wa kuthibiti ujengaji wa hovyo hovyo na pia hakuna mitaro ya kuaminika ingawa tumezungukwa na bahari. Toka afe marehemu Iddi Milan nani anasimamia michoro na udumishaji wa makaro zanzibar?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...