Na Bashir Yakub
Sheria ya Uwekezaji
ya Mwaka 1977 imehamasisha uwekezaji
kwa wazawa na
wasio wazawa kwa
kuweka mazingira rafiki
kwa wajasiriamali katika nyanja
zote. Wapo ambao
wanajua fursa hizi na
wamezitumia kujipatia maendeleo
na wapo ambao
hawajatumia fursa hizi.
Nataka niseme kitu
kimoja kuwa wazawa
wengi wameshindwa kufanikiwa
kwa kutojua uwepo wa fursa. Wengi wangependa
kutumia fursa kama
zipo lakini hawajui ziko
wapi na zinapatikana vipi.
Badala yake wageni
na watu wengine
ambao si wenye
asili halisi ya
Tanzania ndio wamekuwa
wakihabarishana kuhusu fursa
hizi wanazitumia na
wanafanikiwa sana. Wenyeji halisi
wa nchi hii
wanabaki kutazama mafanikio
ya watu hawa
wasijue yanapatikanaje.
Ziko fursa
ambazo zimetolewa na serikali na
kuainishwa na sheria mbalimbali
mojawapo ikiwa hii
ya kusamehewa kodi kwa bidhaa
zinazoingizwa nchini kutoka
nje ya nchi.
Wafanyabiashara watakubaliana
na mimi kuwa
ikiwa utapata msamaha mzuri
wa kodi bandarini basi unayo nafasi
kubwa ya kutengeneza
faida kubwa katika
biashara yoyote utakayoamua
kufanya.
Mara zote kodi
ndio huwa tatizo. Makala haya yataeleza namna
ya kupata msamaha
wa kodi. Kusoma zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...