Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete aliyeambatana na Mkewe, Mama Salma Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Kenya hapa nchini kufuatia kifo cha Mke wa Rais Mstaafu wa Kenya, Mhe. Nwai Kibaki, Mama Lucy Kibaki kilichotokea wiki iliyopita nchini Uingereza. Mwingine katika picha ni Naibu Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Boniface Muhia. Dkt. Kikwete anatarajiwa kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwenye mazishi ya Mama Kibaki yatakayofanyika Nairobi, Kenya.
Mama Salama Kikwete naye akisaini Kitabu cha Maombolezo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dkt. Aziz Mlima naye akisaini kitabu cha maombolezo.
Rais Mstaafu, Dkt. Kikwete (wa pili kutoka kushoto) akimsikiliza Naibu Balozi, Mhe. Boniface Muhia (wa pili kutoka kulia), mara baada ya kumaliza kusaini kitabu cha maombolezo, Mama Salama Kikwete (wa kwanza kushoto) na Balozi Mlima nao wakimsikiliza Naibu BaloziPicha na Reginald Philip

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...