Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela aliongoza kikosi cha wananchi na maafisa wa wanyama pori kumsaka Kiboko aliyevamia mazao ya wananchi na kutishia maisha ya wananchi hao wa kijiji cha Magunga tarafa ya Kiponzelo. 

Kiboko huyo alijificha kwenye eneo ambapo wananchi wa kijiji hicho waliogopa kutembea kufanya shughuli za kilimo. mnamo saa 10 na nusu jioni kiboko huyo alipatikana na kuuawa na baadae wananchi kugawiwa nyama yake. 

Ilikuwa kazi ngumu kumtoa kwenye dimbwi alilo angukia baada ya kuuawa kwa risasi. Kumekuwa na matukio ya wanyama wa porini kuvuka mbuga na kuingia vijijini. wiki mbili zilizo pita simba alionekana kijiji cha Idodi​
Mmoja wa Maafisa Wanyaka pori akitoa maelezo kwa wananchi kabla ya kwenda kufanyika kwa zoezi la kumdhibiti Kigoko huyo.

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akiwa ameambatana na baadhi ya wananchi na Maafisa Wanyama Pori kuelekea aliko Kiboko huyo.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akitoa maelekezo wakati wa kumtoa Kiboko huyo baada ya kuuliwa.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 24, 2016

    Huyu Mkuu wa Wiliya afanye tahadhari. Asipokuwa makini anaweza kupitiliza eneo la mamlaka yake. Itakuwaje iwapo katika kumpiga risasi mnyama huyo ikapitiliza ikaua raia ama askari wanyama? Itakuwa ajali kazini? Kwani hiyo ni kazi yake kubeba na kutumia silaha moto? Awaachie wenye kazi zao kazi hiyo ili kila mtu sheria imlinde kwenye eneo lake la kazi. Thanks God this time around it ended without any incident. It could be worse! Just a thought, but again who cares in Bongo?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 24, 2016

    Sio afanye tahadhari. Serikali iingilie na kukataza. Pakitokea mkasa unadhani atalaumiwa yeye? Watu wataiona Serikali tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...