Tasnia ya filamu Tanzania inazidi kukua kwa kasi, si tu nyumbani hata nje ya nchi watanzania wanazidi kungara.

Safari hii mtoto wa watanzania wenzetu aitwaye Evan Byarushengo amabahatika kupata nafasi ya kushiriki katika filamu ya kimarekani iitwayo THE REAL MVP: The Wanda Durant Story.

Filamu hii inajaribu kuonyesha jinsi mama wa mchezaji nyota wa mpira wa kikapu Kevin Durant alivyohangaika kuwakuza watoto wake mpaka kufikia kuwa mastaa.

Evan anaigiza kama Kevin Durant akiwa mtoto wa miaka 7. Waigizaji wakuu wa filamu hii ni pamoja na Cassandra Freeman anayeigiza kama mama Evan; Pauletta Washington (mke wake Denzel Washington) ambaye anaigiza kama bibi yake Evan na wengine wengi.
Juu, katika clip mojawapo Evan akifanya mazoezi ya kucheza mpira wa kikapu. Nyuma ni director wa filamu George Nelson na wasaidizi wake.
Juu, Evan akiwa anaongea na bibi yake (Pauletta) na mtoto anayeigiza kama kaka yake Kevin aitwaye Tony.
Juu Evan(aliyechuchumaa) akipitia script mbele ya wenzake.
Evan na mwenzake mwishoni walipata bahati ya kuonana na mama yake Kevin ambaye stori ya filamu inamuigiza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 05, 2016

    hii habari nzuri sana kuona mtanzania au mtoto wa watanzania anajitahidi hivi. Mungu azidi kumuongoza huyu mtoto na wazazi wake. As Tanzanians we should be proud of this... Way to go Evan

    ReplyDelete
  2. I love that kid. He is so so smart. Watch for more movies to come ☺

    ReplyDelete
  3. Utanzania ni nini? Je ni ile asili ya wazazi wa mtoto Evan au aina ya utu unaoumbwa kulingana na makuzi katika mazingira halisi ya kitanzania na mahusiano ya kiutu ya kitanzania tofauti na utu mwingine mfano utu wa kikenya ambao tunajitofautisha nao kwa ubinafsi na ukabila? Naona kama mtoto huyo si mtanzania bali ni mmarekani. Labda tuseme ana asili ya kurithi ya kitanzania.Tusiige tabia mbaya ya wakenya ya kung'ang'ania visivyo vyetu!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 06, 2016

    I so happy for you Evan and your family. May the Lord continue opening more opportunities for you.
    I can't wait to watch the movie.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...