Julai
23,2016 Taasisi ya Brigite Foundation imezindua mradi wa taa za solar
katika kituo cha walemavu wa ngozi cha Buhangija katika manispaa ya
Shinyanga kwa ajili ya kuimarisha usalama katika kituo hicho ambacho
sasa kina jumla ya watoto albino 220,wasiosikia 61 na wasioona 33.
Uzinduzi
huo umefanywa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ambapo
mbali na uzinduzi huo wa mradi wa umeme mbadala,watoto katika kituo
hicho walishiriki michezo mbalimbali pamoja na kula chakula cha pamoja
na viongozi wa taasisi ya Brigitte Alfred Foundation na CSI Electrical
Limited.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa mradi huo,Rais na Mwanzilishi wa Brigitte Alfred
Foundation bi Brigitte Alfred alisema mradi huo mkubwa wa kisasa wa taa
za sola utasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha usalama wa watoto hao
katika kituo hicho.
Brigitte
ambaye ni Miss Tanzania mwaka 2012 alisema baada ya kuguswa na hali
iliyopo katika kituo hicho mwaka jana aliomba Kampuni ya Wakandarasi wa
Umeme wa ndani -CSI Kusaidia kufunga umeme katika kituo hicho wakakubali
na hatimaye leo mradi huo umezinduliwa.
“Tunaushukuru
uongozi wa CSI Electrical Limited kwa namna walivyopokea maombi yetu na
hatimaye kuchukua hatua za haraka kwa kutoa msaada huu pia viongozi wa
serikali na chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi kwa ushirikiano wenu
uliosaidia kukamilika kwa mradi huu”,alieleza Alfred.
“Mradi
huu umetimiza na kuunga mkono malengo ya Millenia namba 7 inayolenga
upatikanaji wa nishati salama “Affordable and clean energy”,tunatarajia
mradi huu utahamasisha na kuchochea ari ya wanafunzi katika elimu ya
mazingira na matumizi ya nishati mbadala na watawawezesha kusoma na
kushiriki kwa vitendo katika kufikia malengo ya kitaifa na ya kidunia
kama kizazi na viongozi wa kesho”,aliongeza.
Hata
hivyo alitumia fursa hiyo kuiomba jamii kuunga mkono juhudi za serikali
na kusimamia kauli mbiu ya pamoja ya kuhimiza amani,upendo na
kutokomeza kabisa matukio maovu kwa watu wenye ulemavu wa ngozi na
kuifanya Tanzania endelee kuwa mahala pazuri na salama pa kuishi.
Kwa
upande wake mwakilishi wa Kampuni ya wakandarasi wa umeme -CSI
Electrical Limited Joan Kahwa alisema wamefunga Panel 13 na mradi huo
umegharimu kiasi cha shilingi milioni 75.88.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Huu ni mchango mzuri kwa jamii hii.
ReplyDelete